Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz pamoja na team yake nzima Ijumaa hii waliingia mtaani kwaajili ya kuzaa tiketi za show yake ya Vodacom Wasafi Beach Party itayofanyika Jumamosi hii Jangwani Seabreez Mbezi jijini Dar es salaam.
Diamond akiwa na mteja wake baada ya kumuuzia tiketi
Muimbaji huyo alitua maeneo ya Mlimani City majira ya saa 7 na nusu mchana na kupokelewa na kipindi cha XXL cha Clouds FM ambacho kilikuwa kinarusha tukio hilo live.
Mashabiki pamoja na wadau mbalimbali ambao walijitokeza kwa wingi katika eneo hilo licha ya kuuziwa tikeki na Diamond pia walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusu muziki wake pamoja na WBC.
Katika kipengele cha press play cha XXL ya Clouds FM ambacho kinasimamiwa na DJ D Ommy, mashabiki waliruhusiwa kuchagua ngoma za wasanii wa WCB. Angalia picha.
Ijumaa, 23 Desemba 2016
WCB wasafi wakiwa na clouds leo katika kuuza tiketi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni