Jumatano, 21 Desemba 2016

Wachezaji wapya watakao chemsha ligi kuu bara

klabu zina matarajio makubwa zidi yao hasa kutokana na historia kubwa walizonazo walizopata kwenye klabu walizo wahi kuzitumikia huko nyuma
Mzunguko wa Ligi Kuu Bara ulifunguliwa wikiendi iliyopita kwa klabu zote 16 kushuka dimbani kwenye viwanja tofauti tofauti kila timu ikitafuta pointi tatu muhimu, katika michezo hiyo bado msimamo hukuwa na mabadiliko kwa timu zinazoongoza na zile za mkiani.
Kipindi ligi imesimama kwa ajili ya mapumziko ya takribani mwezi moja klabu zote zilikuwa kwenye mchakato wa kuboresha timu zao sehemu zenye mapungufu ili kujiimarisha kwa ajili ya mzunguko wa pili, wapo wachezaji wapya ambao watang'ara na kadhalika watakao shindwa kuwa na mchango klabuni
Goal inakuchambulia usajili ambao unaweza kushindwa kuwa na msaada kwa klabu zao kwa duru la pili

Emanuel Martin Joseph

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya
JKU ya Zanzibar, straika huyu amesaini kukipiga na Yanga kwa Mzunguko wa pili, na mashindano mengine licha ya kipaji kikubwa alicho nacho Mzanzibari huyu bado ana wakati mgumu kupata namba kikosi cha kwanza Jangwani kulingana na changamoto na ubora wa wachezaji wanaocheza namba anayoimudu yeye.

Juma Liuzio

Yupo Simba kwa mkopo akitokea Zesco ya Zambia, hofu ya wengi juu ya mshambuliaji huyu ni historia yake ya kuwa majeruhi mara kwa mara, muda mwingi amekuwa akiuguza majereha kuliko kucheza, anaweza hasiwe na msaada kwa Simba kama tatizo lake likiendelea kumtesa tena

.
James Kotei

Kutokana na maelezo ya viongozi wa Simba, walisema Mghana huyu amekuja kumpa changamoto Mkude aliyedengua kusaini mkataba mpya ila kuna mashaka na kiungo huyu kama kweli anaweza kumyima usingizi Mkude, kiungo huyu atapata wakati mgumu kuleta ushawishi Msimbazi kwani Simba ni klabu yenye hazina kubwa ya viungo wa kati.

Mrisho Ngasa

Hakuna asiyejua historia ya Ngasa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki, winga huyu wa zamani w\a klabu za Simba na Yanga kitakachompa kikwazo katika klabu yake mpya ya Mbeya City ni kutocheza soka la ushindani kwa muda mrefu tangu aondoke Afrika Kusini
Privacy Policy Terms of Service About Us
Contact Us
Copyright © 2016 Goal.com All rights reserved. The information contained in Goal.com may not be published, broadcast, rewritten, or redistributed without the prior written authority of Goal.com
00:56 LIGI KUU BARA
Goal
NEXT ARTICLE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni