Alhamisi, 29 Desemba 2016

Hii ndio tuzo ya 9 kushinda ronaldo mwaka 2016

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, mwaka 2016 unamalizika kwa kufanikiwa kushinda tuzo 9 katika soka kwa mwaka 2016. Baada ya kufanikiwa kushinda tuzo ya Globe Soccer Award akiwa Dubai.
Ronaldo anashinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa Globe Soccer Award kwa mwaka 2016 inakuwa ni tuzo ya 9, baada ya kushinda tuzo za mchezaji bora wa Ulaya, The World Soccer, Four Four Two, Espy, Di Stéfano Award, Goal.com award, FIFA Club Golden Ball na Ballon d’Or.
Tuzo ya Globe Soccer Award 2016 Ronaldo alikuwa anawania na wachezaji Lionel Messi, Jamie Vardy, Gonzalo Higuaín na Antoine Griezmann, Ronaldo anashinda hii tuzo kwa mara ya nne aliwahi kushinda 2011, 2013 na 2014.
Ronaldo alitangazwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka Ulaya 2016 tuzo hii huwa inaandaliwa na vyombo vya habari 27 vya barani Ulaya, Ronaldo ndio anakuwa mchezaji wa kwanza wa soka kuwahi kushinda tuzo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni