Mchezaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, mwaka 2016 unamalizika kwa kufanikiwa kushinda tuzo 9 katika soka kwa mwaka 2016. Baada ya kufanikiwa kushinda tuzo ya Globe Soccer Award akiwa Dubai.
Ronaldo anashinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa Globe Soccer Award kwa mwaka 2016 inakuwa ni tuzo ya 9, baada ya kushinda tuzo za mchezaji bora wa Ulaya, The World Soccer, Four Four Two, Espy, Di Stéfano Award, Goal.com award, FIFA Club Golden Ball na Ballon d’Or.
Tuzo ya Globe Soccer Award 2016 Ronaldo alikuwa anawania na wachezaji Lionel Messi, Jamie Vardy, Gonzalo Higuaín na Antoine Griezmann, Ronaldo anashinda hii tuzo kwa mara ya nne aliwahi kushinda 2011, 2013 na 2014.
Ronaldo alitangazwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka Ulaya 2016 tuzo hii huwa inaandaliwa na vyombo vya habari 27 vya barani Ulaya, Ronaldo ndio anakuwa mchezaji wa kwanza wa soka kuwahi kushinda tuzo
Alhamisi, 29 Desemba 2016
Hii ndio tuzo ya 9 kushinda ronaldo mwaka 2016
Aunt ezekiel aja na kazi mpya 'chrissmass eve'
Mara nyingi kwenye msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya, waigizaji duniani huingiza sokoni filamu zinazoendana na wakati huo. Ni nadra sana kwa waigizaji wa Tanzania kuja na filamu za aina hiyo. Lakini si kwa Aunty Ezekiel, ambaye mwaka huu ameachia filamu iitwayo, Christmas Eve.
Muigizaji huyo na mama wa mtoto mmoja aliyezaa na dancer wa Diamond, Mose Iyobo, ameshirikiana waigizaji wengine wakiwemo Husna Iddy, Lissa Tarimo, Vivian Minja na wengine kucheza filamu hiyo.
“Usiamini kila kitu unachokiona au kusikia….. Kwasababu kila hadithi Ina pande Tatu yao, yako, Na ukweli,….. Christmas eve bonge LA movie iko mtaanii now …. Go get ur og copy,” ameandika muigizaji huyo kwenye Instagram.
Azam yatimua makocha wake
Uongozi wa klabu ya Azam FC, unapenda kuufahamisha umma kuwa umefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mikabata ya makocha wake kutoka nchini Hispania.
Jopo hilo la makocha linaundwa na Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez.
Uamuzi huo umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo jana, na umetokana na mwenendo mbaya wa Azam FC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), ambayo imefikia raundi ya pili hivi sasa.
Azam FC inawatakia kila la kheri na mafanikio mema makocha hao huko waendako na inawashukuru kwa mchango wao wote walioutoa kwenye timu kwa kipindi chote walichokaa, ikiwemo kuwapa taji la kwanza la Ngao ya Jamii mwaka huu kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2.
Wakati huu ambapo uongozi wa Azam FC upo katika mchakato wa kusaka kocha mpya, kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, ambao walianza kazi jana jioni kukiandaa kikosi kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.
Azam FC inapenda kuwaambia mashabiki wake kuwa wawe watulivu katika kipindi hiki kwani uongozi umefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya kuinyanyua timu juu ili hatimaye ushiriki wetu wa michuano mbalimbali uweze kuwa ni wa kiwango cha juu tofauti na hali ilivyokuwa sasa.
Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameingoza timu hiyo kwenye mechi 18 rasmi ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na ku
Mapya yaibuka tukio la nyoka wa ajabu songea ndugu wachukua mzoga wa nyoka na kwenda kuuzika
Tukio la kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba (24) baada ya nyoka aliyekuwa naye kuuawa, limechukua sura mpya baada ya mambo kadhaa kuibuka.
Hayo ni pamoja na familia kudai mzoga wa nyoka na kwenda nao kuuzika nyumbani, jambo lililoendelea kuhusisha suala hilo na imani za kishirikina.
Imeelezwa kuwa familia ilielezwa na mganga wa kienyeji kuwa mwili uliohifadhiwa hospitali, si wa mtoto wao, jambo lililowafanya kuuchukua mzoga wa nyoka na kwenda kuuweka katika mfuko wa sarandusi (kiroba) na kuuzika.
Hata hivyo, mashuhuda walieleza kuwa, familia hiyo ilikikata kichwa cha nyoka na kukizika kivyake na kiwiliwili sehemu nyingine huku mwili wa Komba ambaye naye alizikwa jana, ukizikwa katika kaburi eneo lingine tofauti. Tukio hilo ni la juzi na lilimhusu Komba, mkazi wa Mateka, manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Nyumbani kwao ni kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Songea. Kabla ya maziko, baadhi ya vijana waliokuwa wamebeba jeneza, walikuwa wakikimbia nalo mwendo wa mchakamchaka huku wakiimba “mkimbize mkimbize nyoka awahi asije kudhuru watu wengine”.
Katika maziko hayo, hakuna ndugu aliyeonekana kulia wala hakukuwa na ibada yoyote wakati jina la marehemu linadhihirisha kuwa ni wa imani ya Kikristo. Wakati hayo yakiendelea msibani, baadhi ya watu wake wa karibu walidai alikuwa na tabia ya kucheza na nyoka mara kwa mara.
Hata hivyo, baba mzazi alikana kumuona mwanawe na nyoka. Naye daktari aliyechunguza mwili, alisema kifo cha Komba kinatokana na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali, lakini hakuna jeraha wala alama yoyote iliyoonekana katika mwili huo.
Jumanne, 27 Desemba 2016
Picha:utampenda ray c akiwa na muonekano wa kihindi
Huwenda huu ukawa ndio ujio mpya wa msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva Rehema Chalamika aka Ray C baada ya misukosuko ya hapa na pale katika maisha yake ya muziki.
Muimbaji huyo ambaye amedaiwa kuweza kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kushindwa kwa muda mrefu,wiki chache zilizopita aliweka kambi ndani ya studio ya Wanene kwa ajili ya maandalizi ya ujio wake mpya.
wiki hii amepiga picha zake mpya zinazomuonyesha akiwa na muonekano wa kihindi. Angalia picha.
Madaktari wamuokoa mkulima aliyechomwa na mkuki mdomoni na kutokea shingoni
Kuna msemo usemao hakuna aijuae kesho yake, huku wengine husema kesho ni fumbo hii imetokea mjini Morogoro kwa mkulima na mkazi wa kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na hatimaye mkuki huo kutokea shingoni.
Tukio hilo ni la Desemba 25, mwaka huu, baada ya mtu huyo kujaribu kuzuia vurugu hizo, zilizokuwa zimetokea baada ya wafugaji hao kulisha mifugo yao katika shamba la maharage na mahindi katika kijiji hicho. Umemjeruhi hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kufanyiwa upasuaji kuondoa mkuki huo na kuokoa maisha yake.
Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Sanifa Mdee, alisema walimpokea mgonjwa huyo akiwa na mkuki mdomoni, ulitokea upande wa shingoni na kuanza kumpatia matibabu na kumtoa mkuki huo, ambapo alilazwa wodi namba moja hospitalini hapo.
Habari njema ni kuwa madaktari wamefanikiwa kuutoa mkuki huo na Mtitu anaendelea vizuri.
Mtitu na wengine wanane walijeruhiwa katika vurugu zilizohusisha jamii ya wafugaji wa Kimasai na wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema mpaka jana watu watatu walikuwa wanashikiliwa na Polisi, na msako unaendelea kuwasaka wale wote waliohusika katika kufanya vurugu hizo.
Kutokana na tukio hilo, wananchi wenzake waliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya matibabu. Baadae alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu zaidi ya kuokoa maisha yake.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo, muda mfupi baadaye wafugaji hao walirudi tena kijijini hapo, kwa lengo la kuokoa mifugo yao iliyokuwa imekamatwa, na ndipo walipoanzisha tena vurugu kwa kuwashambulia watu wengi wanane akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na wa Kitongoji.
Watu watano, kati ya waliojeruhiwa, walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kupatiwa matibabu. Diwani wa Kata ya Masanze, Bakari Pilo, akizungumza kwa njia ya simu, alisema hilo ni tukio la tatu kutokea kwenye kata yake katika kipindi kifupi.
Picha:shilole akiwa na mpenzi wake mpya
Shilole akipenda, mashabiki wake hawafichi kitu. Mahaba aliyokuwa akipewa Nuh Mziwanda, sasa yamehamishiwa kwa kijana mwingine, anayefaidi utunzwaji uliotukuka kutoka kwa muimbaji na mjasiriamali huyo.
Shishi na mpenzi wake huyo hawaachani, wanaambatana kama kumbikumbi, kwenye jet hadi kwenye meli wakifaidi upepo wa bahari ya Hindi. Wawili hao walisherehekea sikukuu ya Christmas pamoja na Shishi hakwisha kumdekea mpenzi wake.
Tazama picha zao chini:
Ben wa bongo movie apata ajali
Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho, Ben Branco Selengo amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mbaya ya gari siku ya sikukuu ya Christmas.
Muigizaji Mboto ambaye ni rafiki wa karibu wa Ben, kupitia instagram ameandika:
Ajali ulioipata sio ndogo kwetu sisi wanadam, lakin kwa mungu ni ndooogo sana. Naamin ndogo kwa mungu kwasababu utapona kwa uwezo wake mungu. Utapona tu inshaallah (Benn Blanco Selengo)
Akiongea na Bongo5 asubuhi hii ndugu wa karibu wa Ben kupitia simu ya Ben, alidai Ben alipata ajali mbaya ya gari juzi na hali yake bado ni mbaya.
“Ben hali yake siyo nzuri kusema kweli,” alisema dada huyo aliyejitambulisha kwa jina na Sarah. “Alipata ajali ya gari juzi na hapa tunapozungumza bado yupo Muhimbili hospitali,”
Jumapili, 25 Desemba 2016
Guardiola:messi ni zaidi ya ronaldo
Guardiola amesema yake juu ya mdahalo unaovuma kuhusu mchezaji bora wa dunia baada ya Cristiano Ronaldo kutwaa tuzo ya nne ya Ballon d’Or mwezi huu
Meneja huyo wa Manchester City ambaye anaiandaa timu yake kwa mechi ya Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Hull City Jumatatu, alikuwa na miaka minne ya mafanikio kama bosi wa Barcelona na alimfundisha Lionel Messi – ambaye ni mpinzani mkubwa wa Mreno huyo katika tuzo, na pia bado anaamini Messi ni zaidi ya Ronaldo.
Baada ya kocha wa sasa wa Nou Camp,
Luis Enrique kusisitiza kuwa Messi bado ni mchezaji bora wa dunia huku akiponda maamuzi ya Ballon d’Or kwenda kwa CR7, Mhispania mwenzake naye amemuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano wa mahojiano na waandishi kuhusu mechi ya Hull City dhidi ya Man City, hiki ndicho alichosema Guardiola: “Nakubaliana na Luis Enrique. Messi ni bora, nab ado ataendelea kuwa. Naam ni bora zaidi.
“Kwa sababu anajua namna ya kucheza, namna ya kufunga magoli. Kwa sababu ndivyo alivyo… kwa heshima zote kwa wachezaji wote ambao wameshinda, na shukrani kwa Cristiano, lakini bado Leo yupo juu zaidi.
Privacy Policy Terms of Service About Us
Contact Us
Copyright © 2016 Goal.com All rights reserved. The information contained in Goal.com may not be published, broadcast, rewritten, or redistributed without the prior written authority of Goal.com
12/24/16 LA LIGA
Getty Images
Mwanamuziki wa uk george michael afariki dunia
Mwanamuziki mkongwe wa nchini Uingereza, George Michael amefariki dunia nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 53.
Msemaji wake amedai kuwa mwanamuziki huyo aliyeanza kujipatia umaarufu miaka ya 1980s amefariki kwa amani huko Goring, Oxfordshire.
Taarifa ya msemaji wake imesema: It is with great sadness that we can confirm our beloved son, brother and friend George passed away peacefully at home over the Christmas period. The family would ask that their privacy be respected at this difficult and emotional time. There will be no further comment at this stage.”
Kikosi bora ambacho wachazaji waliocheza yanga na simba
Wengi wamefanya vizuri baada ya kupindukia upande wa pili baada ya kuonekana mzigo upande mwingine
Simba na Yanga zimekuwa na upinzani wa muda mrefu sasa kuanzia ndani na nje uwanja kwa miaka takribani 80 sasa tangu kuanzishwa klabu hizi na hakuna klabu hata moja itapenda kumuona mwenzake akifanikiwa uwanjani na nje ya uwanjani
Ni mara chache sana tofauti na miaka ya nyuma kwa klabu hizi mbili kuuziana wachezaji wao nyota kwa miaka ya 90 kurudi nyuma ila kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuja mbele imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanadinga hawa kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Ungana na makala hii Goal inakuchambulia wachezaji 11 bora walio wahi kukipinga kwenye klabu za Simba na Yanga kuanzia miaka ya 2000 hadi 2016
1.Juma Kaseja
Baada kuwa na kiwango bora ndani ya Simba kwa miaka 10 mlinda mlango huyu aliamua kupindikia upande wa pili mtaa wa Jangwani mwaka 2009 alicheza msimu moja pale kisha kurudi msimbazi kabla ajarejea tena yanga 2013
2.Hassan Kessy
Licha ya usajili wake kukumbwa na sintofahamu nyingi hadi leo, beki huyu wa kulia alifanya kazi nzuri Simba kabla ajageukia upande wa pili wa wapinzani
3.Amir Maftah
Mlinzi bora wa kushoto kuanzia miaka ya 2003 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2010 aliweza fanya kazi nzuri kwa timu zote kwa vipindi tofauti alikuwa bora kwenye ulinzi pia kuanzisha mashambulizi
4.kelvin Yondani
Wengi umfananisha na mlinzi wa zamani wa Manchester United Memanja Vidic hasa kutokana uimara wao wa kuzuia washambuliaji watukutu baada ya maisha mazuri ndani ya Simba kisiki huyu aliamua kukimbilia yanga miaka 4 nyuma na ndiyo klabu a Mayo amepata mafanikio kuliko huko nyuma
5.Nurdin Bakari
Alipata jina ndani ya Yanga kwa miaka 7 kabla ajatua Simba kwenda kumaliza kiwango chake, Bakari ana uwezo wa kucheza kwenye namba mbali mbali
6.Athuman Idd
Alijiunga na Simba akitokea CDA ya Dodoma baada ya msuguano mkali na viongozi wa Mnyama kiungo huyu bora aliamua kusaini na Yanga, chuji ni moja ya viungo bora kuwahi kutokea hapa nchini
7.Mrisho Ngassa
Ngassa amecheza kwa mafanikio makubwa Jangwani kwa miaka yote aliyoitumikia amecheza Msimbazi kwa msimu moja tu kabla ya kurudi tena Yanga
8.Mohamed Banka
Banka amevitumikia timu zote hizi kwa kiwango bora, kiungo huyu fundi wa mpira alifanikiwa kuvuna mafanikio kwenye klabu zote hizo
9.Amiss Tambwe
Kati ya washambuliaji ambao Simba itawajutia kumpeleka kwa mtani wake basi ni Mrundi Tambwe rekodi zake ziko wazi tangu ajiunga na Yanga
10.hamis kiiza
Maarufu kama Diego, Mganda huyu mwenye rekodi nzuri ya ufungaji anakipiga kwenye Ligi Kuu ya Afrika ya Kusini alifukuzwa na Yanga na kuja kuibuka shujaa ndani ya sSmba msimu uliopita
11.Amri Kiemba
Baada ya kutupiwa virago Jangwani kutokana na kushuka kiwango chake kiungo huyu alkuja kuwa mmoja wa nyota bora nchini ndani ya klabu ya Simba sababu ya kiwango kikubwa alicho onesha Msimbazi
Privacy Policy Terms of Service About Us
Contact Us
Copyright © 2016 Goal.com All rights reserved. The information contained in Goal.com may not be published, broadcast, rewritten, or redistributed without the prior written authority of Goal.com
11:51 LIGI KUU BARA
Harmonize afunguka kuhusu penzi lake na wolper
0 COMMENTS
Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amekanusha kuachana na mpenzi wake Jacqueline Wolper baada ya hivi karibuni kuzagaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameachana.
Madai hayo yalichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya malkia huyo wa filamu kudaiwa kufuta picha za mkali huo wa wimbo Bado katika mtandao wake wa instagram.
Akiongea jana katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Harmonize alidai mapenzi yao yapo moyoni na watu wasichanganywe na issue ya kufuta picha instagram.
“Wolper alifuta tu picha za instagram hakufuta mapenzi yetu yapo moyoni,” alisema Harmonize.
Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Matatizo, alidai suala la malkia huyo kufuta picha instagram ni kawaida kwani anaweza kufuta na kuanza kupost mpya.
Wapenzi hao wamebadili utaratibu wa maisha yao kwani huko nyuma walikuwa wanasafiri na kula bata pamoja.
Kipindi cha weekend chart show kinakuja kivingine sasa kuitwa shilawadu
Kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV sasa kutaitwa SHILAWADU. Mabadiliko ya kipindi hicho cha burudani yataenda sambamba na ujio wa Shilawadu Ubuyu Tour ambapo watangaji wa kipichi hicho, mastaa pamoja mashabiki watapata fursa ya kupanda basi hilo la tour na kukutana na mastaa wao huku kipindi kikirekodiwa.
Qwhisar Thomson mmoja kati ya watangazaji wa kipindi hicho
Akizungumza na waandishi wiki hii mmoja kati ya watangazaji wa kipindi hicho, Qwhisar Thomson alisema kipindi hicho kimeenda mtaani ili kutoa shukrani kwa mashabiki pamoja na kuwapa fursa ya kukutana na mastaa ambao wamekuwa wakihojiwa kila siku.
“Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu, mastaa pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa pamoja na sisi kuanzia mwanzo mpaka sasa hivi,” alisema Qwhisar “Lakini katika namna ya kuwashukuru zaidi tunaenda mtaani na tour basi yetu kuwapa fursa mashabiki ya kukutana na mastaa wao pamoja na kuwauliza yale ambayo wamekuwa wakiyauliza kupitia mitandao ya kijamii.,”
Qwhisar alisema tuor ya Shilawadu Ubuyu Tour itaanza Desemba 24 kwa wakazi wa wilaya ya Temeke, baada ya hapo itaingia Kinondoni pamoja na Ilala.
Pia kipindi hicho kimetambulisha bidhaa yake mpya ya ubuyu wenye jina la kipindi chao ‘SHILAWADU’.
Julian draxler sasa ni mali ya psg
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Nchini Ufaransa, imetangaza kufanya usajili wa kiungo mshambuliaji ,Julian Draxler kutoka Wolfsburg kwa mkataba wa miaka minne na nusu kwa ada ambayo inasemekana kuwa ni pauni milioni £34m.
Mjerumani huyo,23, atajiunga rasmi na matajiri hao wa Ufaransa mwezi ujao katika dirisha dogo la usajili.
Jumamosi, 24 Desemba 2016
Ac milan wabeba supercup ya italia yaipiga juve kwa penati
Wachezaji wa AC Milan wakisherehekea na taji lao la Super Cup ya Italia baada ya kuwafunga wapinzani wao wakubwa wa Serie A, Juventus kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Jassim Bin Hamad (Al-Sadd) mjini Doha, Qatar jana. Giorgio Chiellini alianza kuifungia Juventus dakika ya 18 akimalizia kona ya Miralem Pjanic, kabla ya Giacomo Bonaventura kuisawazishia AC Milan dakika 20 baadaye akimalizia krosi ya Suso.
Gianluca Lapadula na Mario Mandzukic walikosa penalti zao kabla ya kipa wa Milan Gianluigi Donnarumma kuokoa vizuri na kuipa timu yake Super Cup ya saba katika historia yao
Ajib kutimkia misri
Msimbazi Simba SC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Misri kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo awali zilidai kuwa Ajibu ameondoka bila kutoa taarifa kwa uongozi wa klabu, lakini baadaye meneja wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amethibisha kuwa uongozi una taarifa na umetoa baraka kwa mchezaji huyo kwenda kutafuta nje ya Tanzania.
“Ajibu kaenda Misri kwajili ya majaribio na kapata ruksa ya viongozi kama ilivyo ada ya klabu ya Simba, Simba haimzuii mchezaji wake akipata timu ya nje,” Amesema Mgosi.
Ingawa Mgosi amesita kutaja timu ambayo Ajibu anakwenda, lakini taarifa zinaeleza kuwa anakwenda katika timu ya Harass El Hadood.
Source: EATV
Ben paul kuanzia 2017 collable nitatoza milioni 10
Unataka kufanya collabo na Ben Pol? Muwahi sasa kabla ya Disemba 31, sababu mwaka 2017, mambo yanakwenda kubadilika.
Ben Pol amesema kuanzia mwakani atakuwa akitoa dola 5,000 kwa kila kolabo ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Kitanzania.
“Kuelekea 2017 bei yangu ya Collabo itakuwa $5000. So kama una project na mimi tuwasiliane before 31st Dec 2016,” aliandika Ben kwenye Twitter.
“Ni kweli, ila kama wimbo ni mkali tunaweza kukaa mezani na huyo mtu akanipa sehemu ya umiliki wa hiyo kazi,” Ben ameiambia Bongo5 baada ya kumuuliza kama amedhamiria kweli.
“Kwanza nataka kupunguza idadi ya colabo ili nifanye chache za walio serious na wanaoweza kupush hizo project. Mfano mtu hawezi kukulipa dola elfu 5 halafu akaiweka ngoma kwenye album, au akaiweka ndani tu,” amesisitiza.
“Pia itasaidia kwangu kufikiria zaidi kwenye hiyo kazi, hakuna mtu atakulipa dola 5 halafu akatarajia disappointment, so ita-benefit kwa pande zote
Salome na pana zaongoza nymbo 10 bora kwa mujibu wa uk gurdian
Gazeti maarufu la Uingereza, The Guardian kupitia tovuti yake, limetoa orodha ya nyimbo 10 zilizokuwa kubwa Afrika mwaka 2016 . Kwenye orodha hiyo, Diamond na Alikiba wamo. Pana ya Tekno wa Nigeria imeshika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Salome ya Diamond na Ray Vanny.
“In the 90s, Tanzanian legend Saida Karoli’s classic Maria Salome was a hit across most of east Africa and was one of the soundtracks to Tyler Perry’s 2013 film, Peeples,” wameandika.
“More than two decades later, a remake by her compatriot Naseeb Abdul Juma – better known in these parts as the singing sensation Diamond Platnumz – has become a hit, too. The 27-year-old’s version features Wasafi Music labelmate Rayvanny and combines some of the best traditional outfits across Africa in its colourful slideshow of a video that has over 10m YouTube views. It’s a Kiswahili extravaganza.”
Kwenye collabo ya Sauti Sol na Alikiba, Unconditionally Bae wameandika: After clinching a nomination for best international act at the BET awards and getting Barack Obama to do the Lipala dance in 2015, frontline Kenyan boy band Sauti Sol’s hot streak continued this year with the stellar monochrome visuals for the a cappella hit Kuliko Jana. Their biggest work was linking with Tanzania’s Alikiba (who signed to Sony Music this year) for the dance number Unconditionally Bae, which has racked up over 4m YouTube views.”
Hii ni orodha nzima:
Tekno – Pana
Diamond Platnumz feat Rayvanny – Salome
Mr Eazi feat Joey B and Dammy Krane – Hollup
Patoranking feat Sarkodie – No Kissing Baby
Babe Wodumo feat Mampintsha – Wololo
Eugy x Mr Eazi – Dance for Me
Kwesta feat Cassper Nyovest – Ngudu
Yemi Alade – Koffi Anan
DJ Maphorisa feat Wizkid, DJ Buckz – Soweto Baby
Sauti Sol and Alikiba – Unconditionally Bae
Ijumaa, 23 Desemba 2016
Hizi bifu zimesumbua sana 2016
Na Dickson dix
TARATIBU mwaka 2016 unazidi kuyoyoma huku zikiwa zimesalia takriban siku 16 tuukaribishe Mwaka Mpya wa 2017. Kumekuwepo na matukio mengi katika ulingo wa burudani nchini na kimataifa. Moja kati ya mambo yaliyotikisa mwaka huu ni bifu za wasanii mbalimbali hapa nchini, Afrika Mashariki na duniani kwa jumla. Cheki bifu zilizotikisa kinoma noma.
OMMY DIMPOZ Vs DIAMOND
Kwa zaidi ya miaka mitatu hivi, bifu kubwa ya Diamond ambayo wengi wamekuwa wakiifahamu ni ile iliyopo kati yake na Ali Kiba. Lakini juzi kati, imebainika kuwa Diamond ameingia katika bifu na Ommy, ambaye alikuwa mshkaji wake wa karibu. Chanzo cha bifu hilo ni mambo ya kimasilahi zaidi na kutotendeana haki kipindi cha nyuma. Hata hivyo, mzizi ulijikita zaidi baada ya Ommy kuanzisha uhusiano wa ukaribu na Wema Sepetu baada ya kubwagana na Diamond.
Ommy alionekana kuwa karibu na Wema na hata akaishia kumtumia katika wimbo wake wa ‘Wanjera’, jambo ambalo linatajwa halikumfurahisha baba Tiffah.
Hata hivyo, Ommy amezidi kumtia kichefu chefu Baba Tiffah baada ya hivi majuzi kuungana na hasimu wake Ali Kiba na kuachia kolabo ya ‘Kajiandae’. Siku kadhaa baadaye, Diamond alichia kolabo yake na Rich Mavoko ‘Kokoro’ na baadhi ya mashairi yanadaiwa kuwa ni ya kumlenga Ommy.
Mara tu baada ya kutoka kwa ngoma hiyo, Ommy na Diamonds walianza kurushiana cheche za maneno kila mmoja akimkashifu mwenzake kwa ishu mbalimbali. Ommy alidai muziki wa Diamond ni wa kijanja janja na kwamba, hununua ‘views’ kwenye Youtube ili kumwezesha kutengeneza mkwanja.
Malumbano hayo yameendelea na hivi majuzi kwenye mahojiano ya redioni, Diamond kafunguka kuhusu jitihada zilizowahi kufanywa na Ommy ili kumaliza bifu lao ikiwemo kumpigia simu na kumtuma meneja wake Sallam azungumze na Diamond, kitu ambacho mzee wa ‘Wanjera’ kakanusha.
“Kashatuma watu wengi sana, kashamtuma Sallam na alishanipigia simu nikashindwa kupokea, nitaongea naye nini? Mipaka ilishavuka halafu mimi ni Mwislamu. Sina matatizo na watu ndiyo maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa,” alisema Diamond.
Hata hivyo, kupitia Twitter, Ommy alikana: “Aisee kumbe Sallam kila siku unavyonibembeleza tuyamalize na mwana (Diamond) kumbe nakutuma, kweli nyie profeshenooo,” alitwiti Ommy
.
VISITA Vs GRAND PA RECORDS
Ni bifu nyingine ambayo ilionekana kumlenga moja kwa moja mmiliki wa Grand Pa Records, Reffigah huko nchi jirani ya Kenya ambaye katika busara zake aliamua kusalia kimya.
Hii ni baada ya produsa wake matata aliyekuwa amemtunuku cheo cha Naibu Rais wa Grand Pa, Vista kuikacha lebo hiyo akidai kuwa jamaa alikuwa akinufaika kwa huduma zake huku yeye akibakia kapa. Kuondoka ghafla kwa Vista mmoja wa watetezi sugu wa lebo hiyo, kuliwashtua mashabiki wengi kwani alionekana kuwa karibu sana na Reffigah.
Licha ya Reffigah kuupiga uzi mdomo wake kuhusu hili, vyanzo vimearifu kuwa tatizo lilitokana na Visita kuuza beats za ngoma ya msanii chipukizi ndani ya lebo hiyo pasi na idhini ya Reffigah.
Visita anaamini alistahili kwa sababu yeye ndiye amekuwa akitengeneza beast pale na baada ya kuondoka aliungana na mwenzake Kenrazy, aliyeikacha lebo hiyo pia na kuunda yao Hela Records. Vita hiyo ilitikisa nchi jirani, pia moshi wake kufuka huku nchini hasa kwa wasanii waliojihusisha na lebo hiyo.
KANYE WEST Vs JAY Z/SNOOP DOGG
Rapa Kanye kwa sasa yupo katika hali mbaya ya kiakili kwa kile kinachodaiwa kusababishwa na msongo wa mawazo. Matatizo katika ndoa na kutengwa na rafiki yake wa siku nyingi, rapa mkongwe Jay Z imeonekana kumwathiri sana Kanye.
Siku kadhaa zimepita Kanye alilazimika kusitisha ziara ya shoo zake ya Siant Pablo na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ya kiakili na kisaikolojia.
Katika kumbi nyingi ambazo alipanda kutumbuiza kwenye ziara yake hiyo kabla ya kukatiza, Kanye amekuwa akimtupia madongo Jay Z kwa kumtelekeza na hata kuacha kabisa kwenda kumtembelea kama ilivyokuwa hapo zamani.
Hata hivyo, kambi ya Jay Z imesema tangu Kanye afunge ndoa, alibadilika na hasomeki kabisa na ndiyo chanzo cha yeye kujiweka mbali naye.
Ukimweka pembeni Jay Z, Kanye pia amekuwa akiwakashifu wakongwe wengine wa hiphop akiwemo Snoop ambaye naye juzi alimtemea shombo;
“Mimi huvuta bangi ila haiwezi ikakufanya utamke maneno kama yale, sijui Kanye anavuta nini kiasi cha kumfanya apande jukwani na kuanza kutukana watu wasiojihusisha na mambo yake bila mpango,” Snoop alicharuka kwenye kipande cha video alichorekodi na kutupia Instagramu.
FEMI ONE Vs NJERI/SOSOUN
Mwishoni mwa Oktoba rapa wa kike Femi One ambaye muziki wake umeanza kutamaba Afrika Mashariki aliingia studio na kuachia distraki ‘Pilau Njeri’ akiwachana marapa wenzake wa kike. Licha ya yeye kudai aliwalenga marapa wenzake kwa kuzembea kazini na wachache kuendelea kushika chati kwenye ‘game’ akiwemo Wangechi, wanaoendelea kufanya muziki huku akionekana kumlenga zaidi rapa Njeri, ambaye kazi zake nyingi anazifanya kwa lugha ya Kikuyu.
Kwenye mahojiano, Femi One alikanusha kuwa traki hiyo ilimlenga msanii huyo na kusisitiza kwamba, ilikuwa ni ya kuwazindua wenzake wanaosinzia ili wainuke na kukaza.
“Wamelala, hiyo ngoma ilikuwa ni ya kuwachangamshe warudi studio kwa sababu kumenyamaza sana,” Femi One alidai.
Hata hivyo, baada ya wiki mbili tu, Njeri alijibu distraki hiyo ya ‘Pilau Njeri’ na ‘Conoka’ ambapo katika mashairi yake alimchana Femi kuanzia fasheni, maumbile na usanii wake.
Ila ilibainika kuwa wawili hao walianza kuwa na chuki ya kimya kimya baada ya menejimenti ya Njeri kumtokea Femi One kwa ajili ya kufanya kolabo, lakini hasimu wake huyo akamyeyusha.
Kwa upande wa Sosoun, alisema hana uhakika ikiwa kweli Femi One alikuwa akimlenga ila kama ndivyo ilivyo basi kama akiamua kumjibu basi itakuwa ndio mwisho wa taaluma ya mwenzake huyo.
Sosoun aliongeza kwamba huwa ana heshima sana kwa wanawake na kabla ya kujibu lazima awe na uhakika kuwa Femi One alimlenga yeye.
Hata hivyo, pamoja na yote kazi hiyo iliwapa fursa wasanii wengine wa kike chipukizi kutoka.
Serikali yapiga marufuku vitoweo kutoka nje
Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha.
Marufuku hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na kituo cha EATV, ilipotaka kupewa ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.
Naibu waziri huyo alisema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama. Aidha aliwataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.
BY: EMMY MWAIPOPO
WCB wasafi wakiwa na clouds leo katika kuuza tiketi
Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz pamoja na team yake nzima Ijumaa hii waliingia mtaani kwaajili ya kuzaa tiketi za show yake ya Vodacom Wasafi Beach Party itayofanyika Jumamosi hii Jangwani Seabreez Mbezi jijini Dar es salaam.
Diamond akiwa na mteja wake baada ya kumuuzia tiketi
Muimbaji huyo alitua maeneo ya Mlimani City majira ya saa 7 na nusu mchana na kupokelewa na kipindi cha XXL cha Clouds FM ambacho kilikuwa kinarusha tukio hilo live.
Mashabiki pamoja na wadau mbalimbali ambao walijitokeza kwa wingi katika eneo hilo licha ya kuuziwa tikeki na Diamond pia walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusu muziki wake pamoja na WBC.
Katika kipengele cha press play cha XXL ya Clouds FM ambacho kinasimamiwa na DJ D Ommy, mashabiki waliruhusiwa kuchagua ngoma za wasanii wa WCB. Angalia picha.
Tevez amuoa mpenzi wake wa zamani
Manchester zote, United na City, Carlos Tevez akiwa na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla baada ya kufunga ndoa jana mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez alianza urafiki na Vanesa akiwa ana umri wa miaka 13 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Osca katimkia china sasa ndiye mchezaj ghari
Nyota Mbrazil, Oscar akiwa ameshika jezi ya Shanghai SIPG ya China kufuatia kujiunga nayo kwa dau la Pauni Milioni 52 kutoka Chelsea ya England. Oscar sasa atakuwa analipwa Pauni 400,000 kwa wiki timu hiyo ya Ligi Kuu ya China na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani
Yanga yatoa sare na africa lyon ligi kuu
Na Dickson dix
YANGA imevuna faida ya mgomo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kukamata nafasi ya pili kwa pointi zake 37 baada ya kucheza mechi 17 sawa na Simba iliyo kileleni kwa pointi zake 38. Simba inaweza kuongeza gepu la pointi hadi nne iwapo itashinda dhidi ya JKT Ruvu leo Uwanja wa Uhuru.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na African Lyon walicheza kwa kujihami zaidi kipindi cha kwanza wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.
Mashambulizi ya Yanga leo hayakuwa na nguvu kutokana na kocha Mzambia, George Lwandamina kulundika viungo watano, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Said Juma na Deus Kaseke akitumia mshambuliaji mmoja tu, Amissi Tambwe.
Kiungo wa Yanga, Mzimbabwe Thabani Kamusoko akikosa bao la wazi leo
Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke (kulia) akitafuta maarifa ya kumpira beki wa Lyon, Miraj Adam
Winga wa Yanga, Simon Msuva akimiliki mpira mbele ya beki wa African Lyon
Hata hivyo, ililitia misuokosuko lango la Lyon kuanzia dakika ya tatu baada ya Tambwe kupiga kichwa vizuri akimalizia krosi ya Msuva, lakini mpira ukaenda juu kidogo na dakika ya 33 Niyonzima akapiga juu ya kuikosesha timu yake bao la wazi.
Lyon nayo ilikaribia kupata bao dakika ya 30 kama si mpira wa kichwa wa Thomas Maurice kwenda nje baada ya krosi ya Abdallah Mguhi ‘Messi’.
Kipindi cha pili, timu zote ziliingia kwa malengo ya kutafuta mabao na kuanza kushambuliana moja kwa moja hali iliyonogesha mchezo.
Walikuwa Lyon waliofanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 67 kupitia kwa Ludovic Venance aliyemalizia pasi ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Abdallah Mguhi ‘Messi’.
Venance aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mbao FC ya Mwanza, alifunga bao hilo baada kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Awadh Juma.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Yanga walifanikiwa kusawazisha dakika ya 74 kupitia kwa mkali wake mabao, Amissi Tambwe akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
Yanga wakaongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Lyon kusaka bao la ushindi, huku wachezaji walioingia kipindi cha pili, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya wakiupasua vizuri ukuta mgumu wa wenyeji wao, lakini bahati mbaya hawakupata bao.
Wachezaji wa Yanga walicheza chini ya kiwango chao na dhahiri walionekana kuathiriwa na maandalizi hafifu kabla ya mechi hiyo – hususan kutokana na mgomo wa mazoezi kwa siku mbili, Jumatatu na Jumanne wakishinikzia kulipwa mishahahra yao ya Novemba.
Mashabiki wa Yanga waliwatukana wachezaji kwa kitendo cha kugoma na hawakufanikiwa kuwafanyia fujo kutokana na ulinzi wa askari.
Kikosi cha African Lyon kilikuwa; Youthe Jehu, Baraka Jaffary, Miraji Adam, Halfan Twenye, Hamad Wazir, Hamad Manzi, Hassan Isihaka,Omary Abdallah/Peter Mwalyanzi dk80, Awadhi Juma/ Ludovic Venance dk46, Thomas Maurice/Cossmas Lewis dk82. na Abdallah Mguhi.
Yajnga SC; Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi Hajji Mngwali/ Geoffrey Mwashiuya dk74, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/ Obren Chirwa dk56, Amissi Tambwe, Said Juma na Deus Kaseke/ Emanuel martin dk 65
Alhamisi, 22 Desemba 2016
Picha:vanesa mdee atembelea ma piramid ya misri
Hujaifaidi Misri kama hujatembelea Mapiramidi ya kihistoria yaliyopo nchini humo. Ndicho alichokifanya Vanessa Mdee baada ya kuzulu katika nchi hiyo.
Vee Money ameshare picha tatu akiwa katika eneo la Mapiramidi hayo na kuelezea namna alivyojisikia kuyaona kwa mara ya kwanza.
“I went on a one man tour of the Pyramids of Egypt today. Ticked that right off my bucket list. This picture describes EXACTLY how I feel. REJUVENATED! #CashMadame #Afrika #Egypt #Pyramids #SheKing,” ameandika Vanessa kwenye picha aliyoiweka Instagram.
“Our ancestors were the original shapers of every thought process that make up our whole design today. Our sophistication and innovation dates back to over 7000 years ago, I was reminded today. Yet we lag behind.We need to reclaim our thrones,” ameandika kwenye picha nyingine.
Kuna takriban Mapiramidi 118 au 138 nchini Misri, kwa mujibu wa Wikipedia na mengi yalijengwa kutumika kama makaburi kwaajili ya Mafarao na wake zao enzi za kale.
Mapiramidi ya kwanza kabisa yanapatikana kwenye mji wa Saqqara, kaskazini magharibi mwa Memphis. Miongoni mwao ni Piramidi la Djoser lililojengwa kati ya mwaka 2630 BC hadi 2611 BC.
Lakini Mapiramidi maarufu zaidi ya Misri yanapatikana huko Giza, katika vitongoji vya Cairo. Piramidi la Khufu ndilo kubwa zaidi kuliko yote. Ni ajabu pekee la enzi za mababu, lililobaki kati maajabu 7 ya
Tetesi; nick minaj na fetty wap ni wapenz
Huenda Nicki Minaj amempata mwanaume wa kumrithi Meek Mill aliyempiga chini hivi karibuni. Mwanaume huyo ni Fetty Wap!
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na Nicki Minaj ambavyo vimezungumza na mtandao wa udaku wa MediaTakeOut.com, Nicki ameanzisha uhusiano wa karibu na Wap ambao vimedai ni mapema kuuita wa kimapenzi.
Rafiki wa Nicki ameuambia mtandao huo, “They’re working on projects together, and maybe more, but we’re not ready to call them “dating” or “in a relationship” yet. Let’s see where [Fetty’s] head is at.”
Chanzo kingine kimezungumza na mtandao wa HollywoodLife.com na kudai kuwa Nicki anapenda tetesi hizo ziendelee ili kumnyoosha Meek ambaye anadaiwa kumsaliti na mwanamke mwingine. “She’s hoping it will light the fire under his a** so he realizes that she’s a queen and that he should do something about it,” kilisema chanzo.
Nicki alidaiwa kummwaga Meek walipokuwa wakishereheka birthday ya mrembo huyo huko Turks and Caicos, wiki kadhaa zilizopita.
Aenda jela kisa kubaka mtoto wa miaka 9
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Shabani Hussein (29) baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Hussein amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano. Hukumu hiyo imetolewa Jumatano hii na Hakimu Mkazi, Catherine Kihoja baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Catherine alisema “Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kunithibitishia shitaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,”alisema Hakimu Catherine.
Aidha Hakimu aliongeza kuwa upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha shitaka hilo pasipo kuwa na shaka yoyote.
Wanaomshauri darasa akatae shoo za vichochoroni watampoteza
mdau wa muziki ataikumbuka kwa mwaka 2016. Na hadithi yake ina funzo kubwa katika namna ambayo hit song hupatikana. Pengine nilichojifunza zaidi ni kuwa hakuna formula ya jinsi ya kupata hit.
Kwamba ‘don’t bother, just hit the studio do what you love’ mengine yatajulikana mbele ya safari, right? Kwasababu wakati mwingine ule wimbo ambao msanii aliurekodi kwa kujiachia tu studio kuwapa mashabiki wake zawadi, hugeuka kuwa mkubwa hadi humshangaza yeye mwenyewe. Na wakati mwingine, wimbo ambao msanii huuwekea mikakati mikubwa, kufanya uwezekaji wa kufa mtu na promo nzito, hugeuka kuwa ‘flop’ na ‘disappointment’ kubwa.
Kilichotokea mwaka huu kwa Darassa ni mawimbi ambayo kila kona imeyahisi. Muziki umegeuka kuwa wimbo wa hadhi ya ‘national anthem’ kwa muda mfupi. Ndio wimbo wenye rotation kubwa zaidi nchini kwa sasa. Huwezi kuukwepa. Usipousikiliza kwenye redio, utaona video yake kwenye TV. Usipousikia kwenye baa ya jirani, utausikia kwenye bajaj au bodaboda inayokatiza wakati ukitembea barabarani. Kwa ufupi katika mzunguko wako saa 12 za siku, uhakika wa sikio lako kuguswa na mawimbi ya mdundo wake ni mkubwa, utake ustake au labda uweke pamba sikioni.
Na kwa muda mfupi, Darassa amegeuka kuwa msanii wa rap mwenye show nyingi. Darassa amegeuka ‘hot cake.’ Hivyo inamlazimu kusafiri muda mwingi kwaajili ya kutumbuiza. Mfano siku kadhaa zilizopita alikuwa na show tatu katika mikoa miwili tofauti, Iringa na Shinyanga. Ni katika safari yake ya kutoka Kahama kwenda Kakola mkoani Shinyanga ndipo yeye na timu yake walipopata ajali ambayo kama si rehema za Mungu, angegeuka kuwa #hashtag.
Katika wakati huu ambao Darassa anafanya vizuri, amekuwa akipata ushauri mwingi kutoka kwa watu wanaotaka afike mbalimbali zaidi na kwamba asije siku moja akapotea tena baada ya kufika kwenye kilele cha mafanikio kimuziki. Hofu hiyo haikwepeki sababu kuna mifano mingi ya watu waliowahi kutoa nyimbo za ukubwa huo lakini leo hii wanapumulia mashine.
Miongoni mwa ushauri anaoupata ni kuwa apunguze show anazofanya kwa kuweka dau kubwa zaidi ili kuzichuja. Moja ya waliompa ushauri wa aina hiyo ni Sebastian Ndege, ambaye katika sehemu ya alichomshauri anasema, “Usichukue show za mapromoter uchwara waka dissapoint mashabiki wako kuwatia hasira na kukushusha hadhi. Bora ufanye shows chache lakini za ukweli, with detailed showcase.”
Mwingine ni Le Mutuz ambaye anamshauri kuwa ni muda wa yeye kuanza kuchukua malipo ya shilingi milioni 15 hadi 20. Na pia kuwapa masharti mapromota wa maeneo ya mbali kumtafutia usafiri wa ndege. Kwa upendo, wote, wametoa ushauri unaoweza kumjenga japo mwingine unakuwa ni nje ya uhalisia.
Nakubali kuwa kutokana na alipofika, Darassa hapaswi kulipwa kiasi kile kile kama ambacho alikuwa anatoza miaka miwili iliyopita, lakini hilo linapaswa kwenda kwa process. Ni haraka mno kutoka kulipwa mfano milioni 4 kwa show hadi kuwa milioni 20. Inahitaji justification zaidi ya kuwa na hits mbili kuweza kulipwa kwa ukubwa huo.
Watu wasimjaze maneno Darassa na kuanza ajisikie kuwa anapaswa kuanza kuchukua kiasi kile kile ambacho wasanii kama Diamond au Alikiba wanachukua – kumbuka safari ya wawili hawa na nguvu waliyojikusanyia hadi sasa. Hapo alipofika Darassa, kuna rappers kibao nyuma waliwahi kufika, lakini hawakulazimisha kupaa juu ghafla na kutaka walipwe mamilioni ya shilingi ambayo hayaendani na uhalisia.
Huu ndio muda ambao Darassa anaendelea kujijenga kujitengenezea ukubwa huo wa kutoza fedha nyingi au kuzikataa zile zinazoitwa ‘show za vichochoroni.’ Kumbuka kabla ya kuachia Muziki, hakuwa na ‘demand’ hiyo ya hata kuitwa kwenye utitiri wa show hizo. Show za milioni 3, 4 ndizo zinaweza kumjengea na kumtengenezea mazingira ya kudai shilingi milioni 15 au 20 kwa show moja baadaye. Hizi ni show zinazompa mtaji wa kujitengenezea himaya yenye nguvu itakayompa kiburi ya kukataa milioni 5 ili alipwe milioni 15.
Kuna wasanii wanaofanya vizuri ambao kupata show ya milioni 2 au 3 ni ngekewa, haiwezakani Darassa kuzikataa kisa ametoa hit ndani ya mwezi mmoja. Isitoshe, show za vichochoroni ndizo zinaonesha ukubwa wa msanii na dalili kuwa muziki wake umefika mbali. Ehh, ndiyo, haiwezekani kujiita msanii mkubwa wakati unajulikana mjini tu.
Ushauri wangu kwa Darassa ni kwamba aendelee kuwa mnyenyekevu hivyo hivyo kama alivyo sasa bila kuanza kuweka attitude kuwa hataki kwenda baadhi ya sehemu ambazo hazifikiki kwa ndege. Wanasema Roma haikujengwa kwa siku moja, ama hata mbuyu ulianza kama mchicha.. Ni process, inahitaji muda kutengeneza ukubwa, hauji ndani ya siku moja.
Jumatano, 21 Desemba 2016
Wachezaji wapya watakao chemsha ligi kuu bara
klabu zina matarajio makubwa zidi yao hasa kutokana na historia kubwa walizonazo walizopata kwenye klabu walizo wahi kuzitumikia huko nyuma
Mzunguko wa Ligi Kuu Bara ulifunguliwa wikiendi iliyopita kwa klabu zote 16 kushuka dimbani kwenye viwanja tofauti tofauti kila timu ikitafuta pointi tatu muhimu, katika michezo hiyo bado msimamo hukuwa na mabadiliko kwa timu zinazoongoza na zile za mkiani.
Kipindi ligi imesimama kwa ajili ya mapumziko ya takribani mwezi moja klabu zote zilikuwa kwenye mchakato wa kuboresha timu zao sehemu zenye mapungufu ili kujiimarisha kwa ajili ya mzunguko wa pili, wapo wachezaji wapya ambao watang'ara na kadhalika watakao shindwa kuwa na mchango klabuni
Goal inakuchambulia usajili ambao unaweza kushindwa kuwa na msaada kwa klabu zao kwa duru la pili
Emanuel Martin Joseph
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya
JKU ya Zanzibar, straika huyu amesaini kukipiga na Yanga kwa Mzunguko wa pili, na mashindano mengine licha ya kipaji kikubwa alicho nacho Mzanzibari huyu bado ana wakati mgumu kupata namba kikosi cha kwanza Jangwani kulingana na changamoto na ubora wa wachezaji wanaocheza namba anayoimudu yeye.
Juma Liuzio
Yupo Simba kwa mkopo akitokea Zesco ya Zambia, hofu ya wengi juu ya mshambuliaji huyu ni historia yake ya kuwa majeruhi mara kwa mara, muda mwingi amekuwa akiuguza majereha kuliko kucheza, anaweza hasiwe na msaada kwa Simba kama tatizo lake likiendelea kumtesa tena
.
James Kotei
Kutokana na maelezo ya viongozi wa Simba, walisema Mghana huyu amekuja kumpa changamoto Mkude aliyedengua kusaini mkataba mpya ila kuna mashaka na kiungo huyu kama kweli anaweza kumyima usingizi Mkude, kiungo huyu atapata wakati mgumu kuleta ushawishi Msimbazi kwani Simba ni klabu yenye hazina kubwa ya viungo wa kati.
Mrisho Ngasa
Hakuna asiyejua historia ya Ngasa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki, winga huyu wa zamani w\a klabu za Simba na Yanga kitakachompa kikwazo katika klabu yake mpya ya Mbeya City ni kutocheza soka la ushindani kwa muda mrefu tangu aondoke Afrika Kusini
Privacy Policy Terms of Service About Us
Contact Us
Copyright © 2016 Goal.com All rights reserved. The information contained in Goal.com may not be published, broadcast, rewritten, or redistributed without the prior written authority of Goal.com
00:56 LIGI KUU BARA
Goal
NEXT ARTICLE
Ccm dar wampongeza magufuli
Chama cha mapunduzi mkoa wa dar es Salaam kimempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa uchapakazi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, lakini pia kwa kuendesha vyema vikao vya kamati kuu ya chama hicho.
Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
“Rais Magufuli ameendesha vikao kwa muda mfupi, lakini kwa mafanikio makubwa na sisi kama CCM mkoa tutahakikisha tunashirikiana kwa karibu zaidi na viongozi wa taifa walioteuliwa hivi karibuni,” alisema Simba.
Aliongeza kuwa pamoja na Rais Magufuli kuendesha vikao hivyo kwa muda mfupi, lakini ameweza kutoa maamuzi mazito yenye lengo la kukijenga chama hicho kwa siku moja.
Arsenal kumkosa tena julian draxler
Mshambuliaji Julian Draxler ambaye alikuwa akifukuziwa na klabu ya Arsenal yupo njiani kujiunga na mabingwa wa Ufaransa PSG.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshakubali mkataba wa miaka minne kukipiga PSG ingawa klabu yake ya Wolfsburg imesema kuwa mchezaji wake huyo hataondoka bila ya paundi milioni 34.
Julian Draxler ana miaka 23 na amekuwa akiwindwa na Arsenal kwenye kila dirisha la usajili linapowadia.
Kendricky lamah: obama akiondoka ndo mwisho wa wasanii kuingia ikuru
Rapper wa Marekani, Kendrick Lamar amedai kuwa kuondoka kwa Rais Barack Obama madarakani ndio utakuwa mwisho wa wasanii kuingia Ikulu.
Lamar amesema kuwa wasanii wanatakiwa kumpatia heshima yake Rais huyo kwa kuwakaribisha Ikulu.
“I think the world, not just hip-hop owes him,” Lamar ameliambia jarida la XXL. “We all have to give him his credit due for even allowing us into the building. We would probably never get inside that house ever again. Think about it like that. Rick Ross, Cole, Nicki Minaj, he really went for us to come experience it. This is something our grandparents always wanted to see, never thought in a million years, but [we can] pass it down to our generation.”
“You look at him as such a high figure in the world, but for him to embrace you and have a connection with you further than just being the President and make you feel like an actual friend. That’s probably the best moment and one of his best characteristics. Basically watching him interact with my mother, my little niece, myself as a human, I think that’s the greatest thing,” ameongez
Diamond aja na rihana na rick ross ni collable mpya izo
Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alitease ujio wa ngoma ambazo amewashikirisha wanamuziki heavyweight wa Marekani, Rick Ross na Rihanna.
Jumatano hii kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, meneja wake, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo. Sallam alidai kuwa collabo na Rick Ross imeshakalimika, huku ile ya Rihanna ikiwa kwenye hatua za mwisho kwakuwa tayari CV na historia ya Diamond imeshatumwa kwa uongozi wake kuweza kufikiwa maamuzi ya mwisho.
Kuhusu nyimbo alizoshirikishwa Diamond, Sallam alisema mwakwani itatoka ngoma aliyoshirikishwa na Burna Boy na Cassper Nyovest huku pia Dj Van wa Morocco akimshirikisha pamoja na msanii mkubwa wa Dubai.
Alidai kuwa kutokana na ubusy alionao hitmaker huyo wa Salome, imekuwa ngumu kupata muda wa kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Jamaica, Alaine, wimbo alioshirikishwa na msanii wa Ivory Coast Serge Beynaud pamoja na kukamilisha wimbo anaoshirikishwa na rapper namba moja wa Cameroon, Stanley Enow.
Pia alidai kuwa Diamond atatumbuiza kwenye tuzo CAF 2016, Alhamis ya January 5, 2017 mjini Abuja, Nigeria na pia kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (Total Africa Cup of Nations),itakayofanyika nchini Gabon
Baroteli alimwa kadi nyekundu dakika ya mwisho
Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli (kushoto) akimsikiliza refa (kulia). Balotelli alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya mwisho katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya wenyeji, Bordeaux baada ya kumchezea vibaya beki Igor Lewczuk usiku wa jana timu hizo zikitoka sare ya 0-0 PICHA ZAIDI
Yanga yapewa wababe wa comoro ligi ya mabingwa
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za awali za michuano ya klabu Afrika mwakani, Kombe la Shirikisho Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa na wababe wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Ngaya de Mbe ya Comoro.
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam FC wao wataanzia Raundi ya kwanza ambako watamenyana na mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.
Yanga wataanzia ugenini wikiendi ya Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano wikendi ya Februari 17 hadi 19, mwaka huu.
Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.
Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza. Na Yanga wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.
RATIBA KAMILI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
RATIBA KAMILI KOMBE LA SHIRIKISHO 2017
Jumamosi, 17 Desemba 2016
Darasa ..roma...kala na stamina wanastahili ufalme
Kwa mujibu wa Afande Sele, Darassa, Roma, Stamina na Kala Jeremiah, ni rappers anaoweza kuwakabidhi taji lake la Mfalme wa Rhymes.
Afande amedai kuwa kama shindano hilo likirudi tena, vijana hao wanaweza kuwa washindani sahihi kwa sasa.
“Naumizwa kuona kwamba Mfalme wa Rhymes ni tukio ambalo halifanyiki tena wakati watu wanataka lifanyike,” Afande alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM. “Kwahiyo kipindi fulani tulikuwa na uhaba wa rappers wazuri lakini kipindi hiki kuna rappers wazuri kuanzia akina Darassa, Roma, Stamina, Kala wengi,” aliongeza.
“Kwahiyo Darassa, Roma, Stamina sizungumzii kufanya kazi, lakini naweza kuwapa hata ufalme wa rhymes.”
Mfalme wa Rhymes ni shindano lililofanyika mwaka 2004 na kuhusisha rappers mbalimbali wakiwemo Jay Moe, Profesa J, Inspector Haroun, Solo Thang, Madee, Mwana FA, Mandojo na Domokaya, Soggy Doggy na Dully Sykes aliyejitoea siku chache kabla ya shindano.
Afande Sele alishinda shindano hilo na kuzawadiwa gari
Hakuna ugonjwa wa zika nchini
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa Zika nchini Tanzania na hakujawahi kupatikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.
Hayo yamesemwa Jumamosi hii na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.
“WHO inafanya kazi na wizara ya afya kufuatilia taarifa za magonjwa unaofanyika kila siku katika maeneo yote ya afya, na taarifa huletwa wizarani kisha tunashirikishwa ili kutoa katika tovuti yetu, nachoweza kusema hatujapata taarifa za magonjwa ambazo zinazoonyesha dalili za mgonjwa yoyote mwenye zika Tanzania,” amesema Dk Saguti.
Pia, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya ina mfumo maalum wa kupata taarifa za magonjwa na hakuna taarifa iliyoonyesha uwepo wa ugonjwa wa zika “Hakuna mgonjwa yoyote wa Zika Tanzania, narudia mara ya pili hakuna mgonjwa wa zika Tanzania.”
Ajinyonga kisa ugumu wa maisha
Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti mkoani Rukwa, likiwamo la mmoja kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai ya ugumu wa maisha.
Katika tukio la kwanza lililotokea usiku wa kuamkia juzi, mkazi wa kijiji cha Chipu Manispaa ya Sumbawanga, Ignas Mambi (52) alijiua kwa kujinyonga.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Deus Masanja, alisema chanzo cha kujiua kwa mtu huyo kinadhaniwa kuwa ni ugumu wa maisha.
Alisema mara kwa mara marehemu alikuwa akilalamikia ugumu wa maisha, huenda ndiyo sababu inayodhaniwa kuchukua uamuzi mgumu na kujinyonga porini katika mti kwa kutumia kamba ya katani.
Katika tukio la pili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alisema lilitokea Desemba 13, saa tano asubuhi katika kijiji cha Kanyezi, wilayani Kalambo.
Katika tukio hilo, Kamanda Kyando alisema bibi kizee Noelia Pintilila (80) aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.
Kyando alisema mtuhumiwa baada ya kutenda kosa hilo, alikimbia kusikojulikana na kwamba alimuua bibi huyo kutokana na kuwa mtuhumiwa alikuwa akianguka kifafa na mara kwa mara alikuwa akimtuhumu bibi huyo kuwa ndiye anayemloga.
Kutokana na kitendo hicho, Kyando aliwasihi wananchi wa mkoa huo kuachana na imani za kishirikina na kujichukulia sheria mikononi kwa kuwa zimekuwa chanzo cha vifo vya watu wengi.
Soucre: habarihotz