Je! Usajili wa Ndidi kutoka Genk una madhara yoyote kwa maisha ya soka ya Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu hiyo ya Ubelgiji?
Leicester City hatimaye wametangaza rasmi usajili wa Wilfred Ndidi kutoka Genk
kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 baada ya kibali cha kufanya kazi Uingereza kuidhinishwa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria alifaulu vipimo vya afya kujiunga na Leicester mapema wiki hii na alikubari vigezo na masharti kusaini mkataba wa miaka mitano.
Je! Usajili wa Ndidi kutoka Genk una madhara yoyote kwa maisha ya soka ya
Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu hiyo ya Ubelgiji?
Ni wazi kama Samatta alifikiria kuuzwa dirisha la uhamisho wa Januari uwezekano wa yeye kuondoka Genk ni mdogo, kwani klabu haiwezi kukubali kupoteza mchezaji mwingine zaidi mwenye uwezo.
Kwa upande mwingine kutupiwa virago kwa kocha aliyemsajili Samatta kunaweza kuwa moja ya mambo yanayomsukuma Samatta kutamani kuondoka Genk kwani hana uhakika kama ataweza kumshawishi kocha mpya, lakini wazo la kuondoka halitakuwa rahisi kutimia kufuatia kuondoka kwa Ndidi aliyetua Leicester.
Ndidi, ambaye uchezaji wake umefananishwa na ule wa nyota wa zamani wa Leicester N’Golo Kante yupo tayari kucheza mechi za wikiendi za Kombe la FA dhidi ya Everton baada ya kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa klabu yake mpya kwa mara ya kwanza Alhamisi.
“Kila kitu kuhusu kibali cha kazi kipo sawa,” meneja Claudio Ranieri aliwaambia waandishi. “Amefanya mazoezi leo. Yupo tayari kwa mechi ya Jumamosi, na mambo yote yako poa. Sina uhakika [kama atacheza]. Ngoja niendelee kumchunguza katika mazoezi. Leo ilikuwa mara yake ya kwanza. Nadhani kesho nitamwangalia zaidi na kisha nitaamua.
“Ni mchezaji mwenye mvuto na mwenye mustakabali angavu. Ni mrefu na anaruka vizuri sana kwa ajili ya mipira ya kichwa, hukimbiza mpira haraka na mwepesi kutafuta mpira.
“Tumemfuatilia sana na tunatumai kwa haraka atawavutia mashabiki. Ni mchezaji mwingine tofauti na [Kante] – tofauti kabisa. Timu nyingi kubwa zilimtaka, lakini akapendelea kujiunga nasi ili aimarike zaidi.”
Jamie Vardy pia anatarajiwa kucheza mechi hiyo ya Kombe la FA katika uwanja wa Goodison Park baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu, wakati Islam Slimani akiwa bado hajapona vizuri kupangwa kwenye kikosi.
Privacy Policy Terms of Service About Us
Contact Us
Copyright © 2017 Goal.com All rights reserved. The information contained in Goal.com may not be published, broadcast, rewritten, or redistributed without the prior written authority of Goal.com
22:04 TANZANIANS ABROAD
Getty
NEXT ARTICLE
Ijumaa, 6 Januari 2017
Ndidi atimkia leicester je samatha?
Jcb awaponda mashabiki wake baada ya kumkejeri kwanini katemblea ofisi za WCB
Rapper JCB amewashangaa baadhi ya mashabiki wa hip hop waliomkejeli baada ya kuzitembelea ofisi za WCB hivi karibuni. Akiwa kwenye ofisi hizo, JCB alipiga picha na Ray Vann na Babutale.
“Dah wapenda #HipHop ni watu wa ajabu sana eti kupiga picha na baadhi ya wasanii kutembelea studio flani kwao ni kosa,” ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook.
“Wakati huo huo hao wanaojiita #Wanaharakati wa #HipHop hana mchango wowote wa kumsaidia huyo msanii wao wanao mwita mwana Hip hop kama kuja kwenye show kununua cd kununua tshet.”
“Wana subiri tudate au tuvute unga ndo watuongelee tena kwa mabaya….wacheni hizo nyie hizi ni picha tu mnachanganyikiwa na kutukana sasa hilo lingoma likishuka itakuaje.”
Mbuyu twite atua omani
Baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Yanga mchezaji Mbuyu Twite ambaye anaweza kucheza kama kiungo amejiunga na
timu ya Fanja ya Oman.
Twite amesha anza mazoezi na timu yake hiyo ya mjini Muscat Oman, Twite aliutumikia klabu ya Yanga kwa miaka minne, mchezaji mwingine ambaye ni Mtanzania anayeichezea Fanja ni mshambuliaji Danny Lyanga wa Simba ambaye yuko kwa mkopo katika timu hiyo.
Ujumbe wa mehrez baada ya kushnda tuzo
Ni furaha kwa kila mtu pindi mchango wake unapoonekana na kupewa zawadi – ndicho kilichomtokea Riyad Mahrez usiku wa Alhamisi hii baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa kuwabwaga washiriki wengine akiwemo Pierre-Emerick Aubameyang na Sadio Mane.
Mahrez ambaye ni mchezaji wa Algeria amewashukuru mashabiki wote duniani kutokana na kuwa na msimu mzuri kwa mwaka jana na kufanikiwa kuisaidia timu yake ya Leicester City kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza.
Kupiti kwenye mitandao yake ya kijamii, mchezaji huyo ameandika, “African ballon d’or … I thank everyone who supporte me around Africa and around the world .”
Hii ni tuzo ya tatu kubwa kushinda kwa mchezaji huyu baada ya ile ya ‘Mchezaji bora wa mwaka ya chama cha wachezaji soka ya kulipwa Uingereza (PFA) na ‘BBC African Player of the Year’.
Dyna nyange kuwania tuzo ya bae uko nigeria
Msanii wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amechaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards 2017 za nchini Nigeria akiwa ni msanii pekee kutoka Tanzania.
Hitmaker huyo wa Komela amechaguliwa katika vipengele viwili ikiwemo kimoja cha BEST AFRICAN ACT akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana), Jah Vinci (Jamaica).
Kipengele kingine anachowania ni BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo anawania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria)
Kipa denis onyango wa mamelod ashinda tuzo hii
Mchezaji wa klabu ya Memelodi Sundowns ambaye ni golikipa Denis Onyango, raia wa Uganda na ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, msimu uliopita wa mwaka 2015 tuzo hiyo alishinda Mtanzania Mbwana Samata.
Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.
A
Aunt ezekiel katuachia funzo juu ya mapenzi
Moja kati ya matatizo ya watanzania, ni kushindwa kusimamia yale tunayoayaamini. Linapokuja suala la mapenzi wengi hujikuta kwenye wakati mgumu hasa ikiwa yule anayempenda anaonekana si wa maana mbele za watu kwa hadhi,kipato na muonekano.
Pengine mwaka 2016 mwanadada Aunty Ezekiel alituachia funzo,ukipenda usiangalie wengine wanaonaje fuata moyo wako na wasipooelewa wengine wataelewa mwisho wa safari.
Miaka michache nyuma ilisemekana mmoja kati ya warembo A-list wa bongo movie Aunty Ezekiel amebeba mimba ya dansa wa kutegemewa wa Diamond Platinumz, Mose Iyobo, haikuaminika na wengi wetu. Sio kwa kuwa Iyobo hatakiwi kupendwa, lahasha ila kwa kuWa imezoeleka mastaa hasa wa bongo movie kudate na watu wenye kipato kikubwa pengine na umaarufu mkubwa. Wengi waliamini Iyobo ni kama amewekwa kupoteza maboya ili watu wasimjue muhusika haswa wa mimba ya Aunty!
Miaka imepita Mose na Aunty wana mtoto wa kike anaitwa Cookie! Unajua nini? Ukipitia kwenye mitandao ya kijamii moja kati ya couple ambaye sasa zinazopostiwa sana ni Mose na Aunty,watu wanawatamani,watu wanaona wanapendezana.
Ingekua Aunty amewasikiliza pengine kusingekuwa na uhusiano. Ingekuwa amemuona kwa jicho wanalomuona wengine pengine penzi lingekufa siku nyingi. Lakini kwa kuwa alimua kuufuata moyo wake na kuamini kuwa yule ambaye wengine wanamuona sio sahihi kwake ndiye haswaa anastahili kukabidhiwa mtima wake,ndio sababu wapo walipo.
Kwa yoyote anayehusika, mapenzi ni baina ya nafsi mbili zinazopendana,ni vema kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi lakini maaumizi yabaki ya kwako. Mwisho wa siku wewe ndo unajua sababu ya kumpenda uliyenaye. Haijalishi wanasemaje au wanaonaje juu ya uhusiano wako Shika uliposhikilia kama kuelewa,wataelewa mbele wa safari.
I
Huyu ndiye mchezaji bora africa
Shirikisho la soka barani Afrika Caf, January 5 2017 Abuja Nigeria ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na tuzo hizo utolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England Riyad Mahrez alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.
Mahrez ambaye alipata kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa kupata kura 186.
Mahrez ameshinda pia tuzo ya mchezaji bora wa BBC Afrika
Mahrez mwenye miaka 25, aliisaidia tumu yake Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.
Jumatano, 4 Januari 2017
Yanga yawapiga zimamoto bao 2 kombe la mapinduzi
Kikosi cha Yanga kimeendelea kuchanja mbuga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitwanga Zimamoto kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo. Yanga walitawala kila idara huku Zimamoto wakionekana kuwa na hofu kuu dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Simon Msuva ndiye alikuwa shujaa wa Yanga baada ya kufunga mabao yote mawili.
Hata hivyo, Msuva alikosa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50, baada ya kupiga kipa akapangua, alipouwahi na kupiga tena ukagonga mtambaa wa panya na kipa akaudaka.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya pili ya Yanga katika michuano ya Mapinduzi na sasa imefikisha pointi sita na mabao nane katika mechi hizo mbili.
Yaya toure sina mpango wa kuondoka city
Mchezaji Yaya Toure amesema hawezi kutafuta klabu ya kuhamia katika kipindi hichi cha mwezi Januari na badala yake anaangalia zaidi kusaidia klabu yake ya Manchester City.
Toure mwenye umri wa miaka 33, amebakisha miezi sita ya mwisho ya mkataba wake Etihad na yuko huru kuanza kuwasiliana na klabu nyingine.
Lakini amesema: “Kwa sasa naangazia City. Siku za usoni zipo lakini kwa sasa ligi bado haijamalizika.”
Raia huyo wa Ivory Coast alirejeshwa kucheza Novemba baada ya kuwekwa kwenye benchi kwa miezi mitatu kutokana na matamshi ya wakala wake.
Kocha wa City Pep Guardiola alikuwa ameapa kutomchezesha Toure hadi wakala wake Dimitri Seluk aombe msamaha kwa kusema Toure aliaibishwa kwa kutojumuishwa kikosi cha City kinachocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Toure aliomba msamaha kwa niaba ya Seluk mwezi Novemba na amekuwa kiungo muhimu katika timu yake.
Alipo rejea katika mechi yake ya kwanza aliifungia timu yake mabao mawili ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace tarehe 19 Nove
Darasa: diamond ni zaidi ya simba
Hit maker wa wimbo ‘Muziki’ Darassa ameweka wazi maana ya ule mstari wake wa “sio simba, sio chui, sio mamba” kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.
Darasa amedai Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.
“Ningekuwa Diamond nisingejiita simba,” Darassa alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana,”
Pia rapper huyo alidai wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.
“Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah”. Amemalizia
Ferooz :nashindwa kuacha dawa za kulevya
Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.
“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania.
Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.
Young d ajibu tuhuma za kurudia madawa ya kulevya
Hatimaye rapper Young Dee amejibu kwa ufupi kuhusiana na tetesi kuwa amerudi tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Akiandika maneno mafupi sana kwenye post yake mpya ya Instagram, Young Dee amedai kuwa ‘muda utaongea.’
“Time will Tell… Mi sina tatizo na mtu… Tuombeane kheri tu… Siwezi shindana na maneno,” ameandika rapper huyo.
Wiki hii tetesi za kuwa Dee amerejea tena kwenye utumiaji wa dawa hizo zilianza kufuatia maneno ya meneja wake Max mtandaoni. Max alida kuwa rapper huyo ameanza tena kuubwia unga na kwamba amechoka kusumbuka naye.
Tetesi za Young Dee zimekuja katika kipindi ambacho watanzania wanasikitishwa na hali walizonazo Chidi Benz na Nando kutokana na kuathirika vibaya na madawa hayo.
Ney hawatofautisha ali kiba na diamond
Rapper Nay wa Mitego amewatofautisha Alikiba na Diamond kwa style yake tofauti.
Hitmaker huyo wa Sijiwezi ameiambia Planet Bongo ya EA Radio Jumanne hii, kuwa Alikiba ni msanii msanii mzuri lakini Diamond ni mfanyabiashara mkubwa.
“Leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz,” amesema Nay.
Nay ameongeza kuwa watu wengi wamekuwa wakijenga picha kuwa hawezi kufanya kazi na Alikiba kwa kuwa si rafiki yake wa karibu kama ilivyokuwa kwa Diamond.
Mayanga,:nitaipeleka stars afcon 2019
Baada ya Shirikisho la soka Tanzania TFF, kumtangaza kocha wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga, kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kocha huyo amesema yupo tayari kwa kazi hiyo na kuwataka wadau mbalimbali wa mchezo huo kumpa sapoti ili kufanikisha adhamira yake ya kuifikisha mbali timu hiyo.
Mayanga ameongea na mtandao wa Goal amesema, ameupokea kwa mikono miwili uteuzi huo ingawa ni kazi ngumu na yenye kuhitaji ushirikiano wa watu wengi, lakini atajitahidi kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na timu ya taifa kufanya vizuri katika michuano ambayo inaikabili.
“Kuwa kocha wa timu ya taifa siyo kitu cha mchezo kwasababu kuna vitu vingi hasa ukizingatia timu hii kila mtu anasauti nayo kwahiyo nawaomba wadau tushikamane na kupeana sapoti ili kila tutakacho kifanya iwe ni kwa umoja wetu na mafanufaa ya wote,”amesema Mayanga.
Kocha huyo amesema jukumu lake kubwa ni kuhakikisha anakuwa makini katika kuwafatilia wachezaji na kuteua kikosi ambacho kitakubalika na Watanzania wote ili pindi timu inapopata matokeo mabaya watu wasimtupie lawama kocha.
Kocha huyo ameelezea mikakati yake ya kujenga timu imara ambayo itawashirikisha wachezaji wote wanaofanya vizuri kwenye klabu zao za ndani na nje ya Tanzania.
“Niwaombe wachezaji wazingatie na kulinda viwango vyao tunajenga timu yetu sote hivyo nilazima kwanza tuwe na uchungu nao na tuweke wivu wa mafanikio, kwani hatuwezi kuwaona Uganda wanakwenda kushiriki AFCN, na sisi tupo tukiwaangalia,” amesema Mayanga.
Kocha huyo amesema ataendeleza mikakati ya kocha aliyepita Boniface Mkwasa ambaye alikuwa akisisitiza nidhamu na uwanjibikaji wa kila mchezaji kwenye timu yake hivyo hatomuita mchezaji kwenye kikosi chake kutokana na jina lake au umaarufu aliokuwa nao.
Mayanga anachukua nafasi ya Mkwasa ambaye amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja kuifundisha timu hiyo akiwa kama kocha mzawa, akichukua mikoba ya Mholanzi Mart Nooij, ambaye alikatishiwa mkataba wake kutokana na mwenendo mbaya wa timu
Jumatatu, 2 Januari 2017
Azam yashinda moja,kombe la mapinduzi
BAO pekee la mshambuliaji chipukizi, Shaaban Iddi Chilunda limetosha kuipa Azam FC ya Dar es Salaam ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Zimamoto katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo, Chilunda alifunga bao hilo dakika ya 79 akimvisha kanzu kipa baada ya kuipokea kiufundi kwa kifua pasi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Mchezo wa pili wa kundi hilo unafuatia Saa 2:30 usiku wa leo kati ya Yanga SC ya Dar es Salaam na Jamhuri ya Pemba, Uwanja wa Amaan pia, hapa Zanzibar.
TFF yaachana na mkwasa ,salum mayanga kachukua nafasi
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtangaza Salum Mayanga kuwa kocha mpya wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars.
Malinzi amesema leo kwamba hiyo inafuatia aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumaliza Mkataba wake leo.
Majukumu ya Mayanga yatakuwa ni kuandaa kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mechi za kufuzu CHAN.
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 akimrithi Mholanzi, Mart Nooij na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
Katika kipindi chake cha kuwa Taifa Stars, Mkwasa ameiongoza timu katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.
Chini ya Charles Boniface Mkwasa (kulia) Taifa Stars, imeshinda mechi mbili tu kati ya 13, ikifungwa sita na sare tano
REKODI YA MKWASA TAIFA STARS
Tanzania 1-1 Uganda (Kufuzu CHAN, Kampala)
Tanzania 1-2 Libya (Kirafiki Uturuki)
Tanzania 0-0 Nigeria (Kufuzu AFCON Dar)
Tanzania 2-0 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Tanzania 0-1 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Blantyre)
Tanzania 0-2 Afrika Kusini U23 (Kirafiki Johannesburg)
Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Algeria 7-0 Tanzania (Kufuzu kombe la Dunia Blida)
Tanzania 1-0 Chad (Kufuzu AFCON D’jamena)
Tanzania 0-2 Misri (Kufuzu AFCON Taifa)
Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki Nairobi)
Tanzania 0-3 Zimbabwe (Kirafiki
Yanga yapiga mtu ,6-0 kombe la mapinduzi
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
YANGA SC imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kuichapa mabao 6-0 Jamhuri ya Pemba usiku huu Uwanja wa Amaan.
Ushindi huo, unaifanya Yanga iongoze Kundi B, kwa pointi zake tatu sawa na Azam iliyoshinda 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa kwanza jioni ya leo.
Winga Simon Msuva alifungua biashara nzuri dakika ya 19 akiifungia Yanga bao la kwanza kwa kumalizia kona maridadi ya Nahodha, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga mabao mawili mfululizo daakika ya 23 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali na dakika ya 37 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa, Omary Said kufuatia shuti la Msuva.
Msuva tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga baola nne dakika ya 40 akitumia makosa ya kiopa kutoka langoni bila mahesabu.
Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza na mtaji wa mabao 4-0, kocha wa Yanga, George Lwandamina akakianza kipindi cha pili kwa mabadiliko, akimpumzisha kiungo Mzambai mwenzake, Justin Zulu na nafasi yake kuchukuliwa na mzalendo, Said Juma ‘Makapu’.
Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 59 akimalizia krosi ya Juma Abdul, kabla ya kiungo Juma Mahadhi aliyetokea benchi pia kipindi cha pili kuhitisha tafrija za mabao kwa kufunga la sita dakika ya 85 kwa shuti la karibu.
Katika mchezo huo, nafasi pekee nzuri ambayo Jamhuri walipoteza ilikuwa ni mapema atu dakika ya 13 baada ya krosi ya Ahmed Ali kuokolewa na beki wa Yanga Andrew Vincent ‘Dante’ na kuwa kona iliyochongwa na Mohamed omary ambayo haikuza matunda baada ya beki huyo kuokoa tena.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk72, Vincent Andrew ‘Dante’, Justin Zulu, Simoni Msuva/Geoffrey Mwashiuya dk77, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Juma Mahadhi dk66, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke dk66 na Emmanuel Martin.
Jamhuri: Omary Said, Mohammed Mgau, Mohammed Omary, Mohammed Juma, Yussuf Makame, Greyson Gerald, Umry Bagaseka, Mbarouk Suleiman, Mwalimu Mohammed, Ahmed Ally na Mussa Mbarouk.
Watu 23 wafariki ajali ya meli iliyotokea indonesia kwa kuteketea na moto
Watu 23 wamefariki dunia Jumapili hii na wengine 17 hawajulikani walipo nchini Indonesia baada ya kuzuka kwa moto kwenye meli iliyokuwa imebeba watu zaidi ya 200.
Waokoaji wakiendelea na zoezi la kuokoa watu kwenye ajali hiyo
Imedaiwa kuwa meli hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea katika kisiwa cha utalii cha Tidung Island kilichopo Mashariki mwa mji wa Jakarta.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi wa nchi hiyo, Hendrianto Bachtiar ameiambia CNN kuwa watu 194 wameokolewa kasoro 17 ambao bado hawajaonekana lakini pia wanamshikilia nahodha wa meli hiyo kwa ajili ya kupata maelezo zaidi.
“We have detained the captain of the boat, and are now taking his statement,” amesema Bachtiar.
Askali wa nyama pori mbaloni kwa kuua na kuficha maiti
Jeshi la polisi mkoani Dodoma, linawashikilia askari watatu wa wanyamapori wa pori la akiba Swagaswaga wilayani Kondoa, wakituhumiwa kumuua mkazi wa kijiji cha Olimba wilaya ya Chemba kwa kumpiga risasi mgongoni wakimtuhumu kubeba nyama pori.
Akizungumza ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo lilitokea Disemba 31,mwaka jana saa 7:30 mchana katika kijiji cha Selya kata ya Selya wilayani humo.
“Marehemu ambaye hakufahamika jina lake lakini mkazi wa kijiji hicho, alikuwa akiendesha pikipiki huku akiwa amepakia kiroba kilichokuwa na sukari guru ndani yake, lakini askari wanyamapori hao walimhisi amebeba nyama pori na bila kumsimamisha na kumhoji waliamua kutumia bunduki zao kumuua papo hapo,” alisema Kamanda Mambosasa.
Aidha Kamanda huyo amesema baada ya kufanya mauaji hayo, askari hao waliubeba mwili huo kwenye gari walilokuwa nalo pamoja na pikipiki ya marehemu na kiroba cha sukari guru, kisha kwenda kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo la Swagaswaga.
“Baada ya kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo, walichukua pia pikipiki na kiroba na kuvificha kila kimoja mahali pake kwa lengo la kupoteza ushahidi wa tukio hilo”.
Kamanda Mambosasa alisema wakati askari hao wanafanya tukio hilo, walishuhudiwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho ambaye alijificha porini ambaye aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Kondoa.
Wahusika wa tukio hilo ni wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ni George Grefee (26), Chini Paulo (40) na Christopher Waunko (36).
Jumapili, 1 Januari 2017
Harmonize:wcb hakuna chuki
Harmonize amedai kuwa hakuna ushindani ndani ya lebo ya WCB wala chuki tofauti na watu wengine wanavyodhania.
Hitmaker huyo wa Matatizo, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa ndani ya lebo yao hawajawahi kushindana wala wanapotoa nyimbo hawatoi kwa mashindano kati yao ila mashabiki ndio wanaowachukulia hivyo lakini kibiashara kwao inakuwa vizuri.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio yakwao waote.
Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kuda kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake waliopeana kuachia nyimbo zao.